KIINI HALISI CHA SIKU YA VALENTINE NA ONYO KWA WAMASIHI

UTANGULIZI

Siku ya Valentine, inayoadhimishwa tarehe 14 Februari kila mwaka (mwaka huu itakuwa Leo, Ijumaa, 14.2.2025), inaonekana kama siku ya kusherehekea mapenzi, lakini kiini chake halisi kinahusiana na DESTURI ZA KIPAGANI. Wengi hushiriki bila kujua kuwa inatokana na ibada za miungu wa Kirumi kama Lupercus, Faunus, na Cupid, waliodhaniwa kuwa miungu wa uzazi na mapenzi.

Katika Ufalme ya Kirumi, kulikuwa na sherehe za Lupercalia, zilizofanyika tarehe 13 hadi 15 Februari, ambapo wanyama walitolewa kafara, na makuhani walitumia vipande vya ngozi za mbuzi kuwagonga wanawake waliokuwa barabarani, wakiamini kuwa hilo lingewafanya kuwa wenye kupokea mimba kwa urahisi. Cupid, anayeonekana kwenye picha nyingi za Valentine’s Day, ni mungu wa mapenzi aliyedhaniwa kuwa na uwezo wa kumpiga mtu mshale wa mapenzi ili kumfanya apendane na mwingine.

Baadaye, Kanisa la Kirumi lilijaribu kubatiza sherehe hii kwa kuihusianisha na mtu aitwaye Valentine, kasisi wa karne ya tatu aliyedaiwa kuozesha wanandoa kwa siri, kinyume na agizo la Kaisari Claudius II. Inasemekana aliuawa tarehe 14 Februari mwaka 269 BK, na hivyo akaorodheshwa kama mtakatifu wa wapendanao. Hili lilikuwa jaribio la kufunika asili ya kipagani ya sherehe hiyo, lakini msingi wake uliendelea kuwa wa kidunia.

Katika nyakati za kisasa, Siku ya Valentine imegeuzwa kuwa biashara kubwa ya kuuza kadi, maua, chokoleti, na zawadi, ikichochea anasa, tamaa za kimwili, uasherati na ngono kwa hali ya juu sana. Kwa sababu hii, Wamasihi wanapaswa kuzingatia mafundisho ya Maandiko ambayo yanatukanya dhidi ya kushiriki katika sherehe za kipagani na matendo ya giza.

ONYO KUTOKA KATIKA MAANDIKO

1. Kutotembea kama mataifa ya dunia (Waefeso 4:17-19).

2. Kujitenga na upotovu wa dunia (2 Wakorintho 6:14-17).

3. Mambo ya dunia ni ya muda mfupi na huangamia (1 Yohana 2:15-17).

4. Mwili wa mtu ni hekalu la Roho Mtakatifu, lisiwe na uasherati (1 Wakorintho 6:18-20).

5. Uasherati na zinaa ni dhambi kubwa mbele za Elohim – (Waebrania 13:4).

6. Tusiwe sehemu ya mambo yasiyo ya Elohim (Warumi 12:2).

7. Matendo ya mwili ni dhambi na hayana nafasi kwa waaminio – (Wagalatia 5:19-21).

8. Tusijifinze Mambo ya mapagani na mataifa (Yeremaya 10:1-3).

9. Mataifa watoa kafara kwa mataifa si kwa Elohim (1 Wakorintho 10:19-20; Matendo 15:23).

10. Tufwate Amri za Elohim na si maagizo ya wanadamu (Mathayo 15:9).

HITIMISHO

Kwa msingi wa Maandiko haya, ni wazi kuwa Siku ya Valentine sio sherehe inayofaa kwa Wamasihi, kwani inahamasisha anasa, uasherati, usinzi, na ibada zisizompendeza Elohim. Badala ya kushiriki katika mambo yanayompinga Baba wa Mbinguni, ni vyema kujibidiisha katika mafundisho ya kweli ya Biblia na kuishi maisha matakatifu yanayompendeza Yeye. Wamasihi wanapaswa kutambua mitego ya dunia na kuikwepa ili wasianguke katika dhambi ( Ufunuo 18:4).

Mbarikiwe sana..

Somo hili limeandikwa na by Ndugu Mutonga (Pipeline Church, Nakuru, Kenya, East Africa, Africa)

babakevi@gmail.com

+254722-80-80-47

Ruhusa imetolewa kusambaza kwa namna yoyote ile bila malipo.

#NiVizuriKujua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *